Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Saad Mtambule ameitaka jamii kukabiliana na kukemea suala zima la mmomonyoko wa maadili kwenye Mitaa na sehemu wanazoishi. Mheshimiwa Mtambule ametoa wito huo Agosti 7, 2024 katika kikao chake na Viongozi wa dini, Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa, Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Turiani. "Jamii inapaswa kuyaishi maisha ya Kitanzania ili kuenzi maadili na utamaduni wetu ambao kwa kiasi kikubwa umeathiriwa na wimbi la mmomonyoko wa maadili," alisema Mhe. Mtambule.
Aidha, Mkuu wa Wilaya huyo alisema suala la mmomonyoko wa maadili linaathiri nguvu kazi ya Taifa, Serikali imekua ikipambana kuwekeza katika miradi mingi hivyo nguvu kazi inayotarajiwa kunufaika inakosekana hivyo ni muhimu kuilinda.
Kwa upande wake Padri Christian Likoko, alisema kuwa ili jamii yetu iondokane kabisa na janga la mmomonyoko wa maadili tunatakiwa tuzingatie malezi bora kwa Watoto tangu wakiwa wadogo. "Matokeo ya athari za malezi yasiyofaa hupelekea mmomonyoko wa maadili kwa kiasi kikubwa ndani ya jamii zetu," alisema Padri Likoko.
Nae, Kamishina Msaidizi, Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Kinondoni Mtatiro Kitinkwi, alisema jamii inapaswa kutoa taarifa kwa haraka pindi viashiria vya ukatili na unyanyasaji wa namna yoyote ile au matukio yanaendana na mmomonyoko wa maadili watoe taarifa.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.