Kauli hiyo imetolewa leo na Mhe Diwani wa kata ya Kunduchi Mh. Michael Urio kwenye hafla ya uzinduzi wa wiki ya unywaji wa maziwa mashuleni inayoratibiwa na Idara ya mifugo na uvuvi kwa Manispaa ya Kinondoni na kufanyika katika Shule ya Sekondari Kondo.
Amesema kuwa, serikali ya awamu ya tano inayo nia madhubuti na mwelekeo wa dhati katika kuijenga Tanzania ya Viwanda na uchumi wa Kati, hivyo inahitaji jamii ya watu wenye afya thabiti na akili ya kupambanua mambo kwa ufasaha ili waweze kuendana na sera hiyo.
"Maziwa yana virutubisho vyote mhimu vinavyotakiwa katika ujenzi wa mwili na akili hivyo badala ya kunywa pombe na vinywaji vingine tunyweni maziwa kwa wingi ili kuunga juhudi za serikali pia viwanda vyetu vya ndani" ameongeza mhe Urio.
Aidha Quenter Mawinda kwa niaba ya msajili wa bodi ya maziwa amewashauri wanafunzi kutumia maziwa kwa wingi ili kuimarisha afya ya akili na mwili na waweze kuendana na Kasi ya Mhe Rais maana anahitaji vijana wachapakazi walioimara.
Mara baada ya uzinduzi huo , Manispaa ya Kinondoni kupitia idara ya mifugo na uvuvi imegawa maziwa katika shule tano za Sekondari ambapo zaidi ya paketi 350 kwa kila shule zimegawiwa.
Uzinduzi huu unatarajiwa kitaifa kufanyika Mkoani Arusha kuanzia tar 28 mwezi wa tano hadi tarehe 1 mwezi wa sita.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.