Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Daniel Chongolo katika hafla ya upokeaji mabati kutoka kampuni ya ando, yatakayowezesha kuezeka darasa moja katika shule ya msingi Wazo hill.
Amesema kwa juhudi za pamoja kati ya Serikali kwa kushirikiana na wadau katika kuhakikisha miundombinu ya shule, elimu na mazingira vinaboreshwa, kwa hakika taaluma katika Wilaya yeu itapanda.
"Serikali inalengo mahususi la kuhakikisha miundombinu ya elimu inapatikana na inaboreshwa, katika hili ninafurahishwa sana kuona tunao wadau katika Wilaya yetu walio tayari kutuunga mkono, tunawashukuru sana kwa uzalendo mlionao"Amesema Chongolo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya (ando), Bw Godlistern Maimu amesema, kampuni yao imejiwekea utaratibu wa kusaidia jamii kwani wanaamini ndoto za wanafunzi zitafikiwa pale watakapopatiwa elimu bora na katika mazingira mazuri.
Naye Afisa Elimu wa Manispaa hiyo Ndg Kiduma Mageni alipotakiwa kuongea, aliushukuru uongozi mzima wa kampuni ya ando) kwa kushirikiana na Serikali katika kuboresha mazingira ya elimu, na kuahidi kuyalinda na kuyatumia kwa makusudi yaliyokusudiwa.
Katika hatua nyingine Mhe Chongolo ameahidi kutatua changamoto ya vyumba vya madarasa pamoja na ukosefu wa ofisi ya walimu unaoikabili shule ya Msingi Wazo hill kwani kwa sasa ina idadi ya wanafunzi zaidi ya 3000 huku ikiwa na walimu 57 pekee.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.