Mwenyekiti wa Kamati ya Kudhibiti UKIMWI Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Joseph Rwegasira amewataka Wananchi kuzingatia malezi na maadili ya kitanzania ili kujikinga dhidi ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI. Ametoa wito huo katika Kikao cha Kamati ya Kudhibiti UKIMWI kilichofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni Mei, 24 2024. Mhe. Rwegasira amesisitiza utoaji wa elimu kwa Wananchi kuhusu athari za maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na namna ya kujilinda.
"Kuna ongezeko kubwa la maambukizi ya Virusi vya UKIMWI katika jamii yetu hivyo jamii inapaswa ijilinde na ngono zembe hasa kwa Wanafunzi walipo kwenye Shule za Sekondari". Amesema, Mhe. Rwegasira.
Aidha, Diwani wa Viti Maalum Mhe. Grace Mkumbwa amewaomba Wadau wa Elimu kuelimisha jamii namna ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI Mashuleni kwa kuanzisha vipindi na semina mbalimbali ambazo zinatoa elimu ya kujikinga na ugonjwa huo pamoja na kuzingatia maadili.
"Inabidi ziwepo semina za kutosha zinazohusiana na elimu ya kudhibiti maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kwa Wanafunzi hivyo Wadau wa Elimu simamieni maadili ya Walimu kuanzia mavazi mpaka tabia zao kwani wao wanapaswa kuhakikisha Wanafunzi wanafata maadili yaliyo bora". Amesema, Mhe. Mkumbwa.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.