Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Saad Mtambule amewataka viongozi na wafanyabiashara wa masoko yote ya Manispaa ya Kinondoni kuimarisha umoja na mshikamano baina yao ili kukuza shughuli za kibiashara kwenye masoko hayo.
Mheshimiwa Saad amesema hayo leo tarehe 24 Oktoba, 2023 alipokutana na viongozi wa masoko yote ya Wilaya ya Kinondoni pamoja na wafanyabiashara kwa lengo la kujadili na kuhamasisha umoja na mshikamano baina ya viongozi na wafanyabiashara.
Lakini pia Mheshimiwa Saad amewaomba viongozi hao kusimamia, ulinzi, usafi na ugawaji wa maeneo ya kufanyia biashara.
Mkuu wa Wilaya ameongeza kuwa, "Viongozi wachukue mawazo chanya yenye kujenga na kuepusha malumbano kwenye masoko".
Aidha, wafanyabiashara na viongozi hao wametakiwa kuangalia jinsi ya kuendeleza biashara, kukuza masoko na kuimarisha miundombinu kwa kutengeneza mazingira yenye kukidhi mahitaji ya wafanyabiashara na wateja.
Vile vile amewataarifu kuwepo kwa kongamano kubwa la wajasiriamali na wafanyabiashara wa Wilaya ya Kinondoni tarehe 28 Oktoba, 2023 katika viwanja vya Biafra. "Niwaombe wafanyabiashara wote washiriki kongamano hilo ili tuweze kujadili na kutatua changamoto".
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.