Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mheshimiwa Kheri James, amewataka watumishi wa umma kuimarisha mahusiano na mawasiliano kati yao na kwa wananchi katika kutekeleza majukumu yao.
Wito huo ulitolewa katika kikao cha uimarishaji Mahusiano baina ya Watumishi wa Umma na Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kinondoni kilichofanyika Septemba 04, 2024 katika Ukumbi wa Soko la Magomeni.
Aidha Mhe.Kheri James alisisitiza kuwa mafanikio ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo yanategemea kwa kiasi kikubwa ushirikiano mzuri na mawasiliano thabiti kati ya watumishi wa umma na wadau mbalimbali. Pia, alihimiza umuhimu wa kuzingatia uwazi, uwajibikaji, na uadilifu ili kuhakikisha rasilimali za umma zinatumika kwa ufanisi na kwa manufaa ya wananchi wote.
"Kwa namna muundo wa serikali na jamii ulivyo kila mtu anaishi kwa kumtegemea mwenzake,kwa msingi huo mahusiano na Mawasiliano ni agenda ambazo haziepukiki katika kuleta chachu ya maendeleo ndani ya jamii yetu." Mhe. Kheri alisema.
Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, watendaji wa umma, na wawakilishi wa jamii, ambao wote walikubaliana na wito wa Mheshimiwa Kheri James kuhusu umuhimu wa kuimarisha mawasiliano na mahusiano katika kutekeleza majukumu ya kila siku.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.