Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Saad Mtambule amewataka Watendaji na Wakandarasi kuimarisha mahusiano mazuri ili kung'arisha mazingira ndani ya Wilaya ya Kinondoni. Mhe. Mtambule aliyasema hayo Mei 27, 2024 katika Kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni alipokuwa akizungumza na Watendaji wa Kata zote 20 sambamba na Wakandarasi wanaojihusisha na huduma ya utoaji wa taka katika maeneo yote.
"Imarisheni Mahusiano na Mawasiliano mazuri katika kujulishana na kujadiliana jinsi ya kuondoa taka na kumfanya kila mmoja atambue wajibu wake katika kusafisha mazingira. Alisema, Mhe. Mtambule.
Pia, amewataka kuweka kipaumbele katika maeneo yenye masoko na magulio na kuhakikisha taka zinatolewa kwa wakati.
"Wakandarasi na vikundi vya usafi wekeni kipaumbele katika maeneo ya Fukwe, Magulio na Masoko ili kuhakikisha jamii inajikinga na magonjwa ya milipuko".
Aidha, Mkuu wa Wilaya aliwataka Maafisa Mazingira na Maafisa Afya kuhamasisha usafi katika maeneo yote na kusimamia sheria kwa wanaochafua mazingira. Pia, Mhe. Mtambule alizuia utoaji wa vibali vya utupaji wa taka katika maeneo ya Kinondoni na kutaka hatua kali zichukuliwe dhidi yao ikiwemo ulipaji wa faini.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.