Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imezindua Kampeni ya kingatiba dhidi ya magonjwa ya Matende na Mabusha itakayoanza rasmi Disemba 6-10, 2023.
Akiongea wakati wa uzinduzi huo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Songoro Mnyonge amesema kuwa mara kadhaa kampeni nyingi hususani za masuala ya afya, zimekuwa zikipata ukinzani mkubwa kutokana na imani potofu.
"Nawaomba sana Waheshimiwa Madiwani tukawe mabalozi kwa Wananchi kuwaeleza juu ya umuhimu wa kupata dawa kama Kingatiba ya maradhi haya ya ugonjwa wa Matende na Mabusha", amesema Mhe. Songoro.
Aidha, Mhe. Songoro amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya haiwezi kuona Wananchi wake wanateseka kwa vitu ambavyo vinatibika, hivyo basi Wananchi wapewe elimu ili waachane na zana potofu dhidi ya kingatiba na chanjo mbalimbali ikiwepo ya Mabusha na Matende.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.