NI BANDA LA KINONDONI PEKEE UTAZIPATA.
Mboga hizi hupatikana sana sehemu zenye ubaridi kama vile Milima ya Uluguru, na Mikoa ya Kilimanjaro na Mbeya.
Asili ya jina lake ni kutokana na kwamba hushika sana nguo unapojaribu kuyasogelea au kugusana nayo.
Mbegu zake ni nyembamba na zinafanana na binzari na huwa na rangi nyeusi.
JINSI YA KUZIPANDA.
Mboga hizi hazitofautiani Sana na mchicha katika upandaji wake.
Unachotakiwa kufanya ni kuandaa tuta vizuri, weka mbolea, halafu unasia mbegu kwa mstari. Hakikisha mstari kwa mstari ni cm 50.
Mbegu hizi huchukua muda wa siku 5 mpaka saba kuota.
MATUMIZI :
Majani haya ya Mashonanguo hutumika kama Mboga za kawaida.
Wakati mwingine hutumika kama Majani ya Chai.
FAIDA ZAKE :
Majani haya ya Mashona nguo au mboga zinafaida kubwa Sana katika mwili wa Mwanadamu.Kwanza
. Zinatibu Presha
.Huchangamsha mwili,
. Zinatumika kama Juice ya kuongeza damu .
Pamoja na Kutibu vidonda vya tumbo.
Kwahabari hizi na nyingine nyingi, ungana na Mtaalam wa Kilimo Bi. Agness Sirili.
imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.