Hayo yamebainishwa leo na Waziri wa Afya jinsia, wazee na watoto Mh Ummy Mwalimu alipofanya ziara katika hospitali hiyo, na kujionea Mazingira ya utekelezaji wa majukumu yao, changamoto zinazowakabili pamoja na miundombinu yake.
Amesema kwa hospitali hii kutoa huduma chini ya usimamizi wa wizara ya afya ni kufuatia utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Dr.John Pombe Joseph Magufuli tarehe 25/11/2017, alipokuwa akizindua hospitali ya Mloganzila na kutangaza rasmi hospitali za mikoa kuwa chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya
Ameongeza kuwa maagizo hayo yalilenga kuboresha usimamizi na kuhakikisha uwepo mzuri wa mgawanyo wa madaktari unaoepusha mrundikano wa madaktari wengi katika hospitali moja, ukienda sambasamba na moboresho katika maeneo muhimu kama vile miundombinu kwa ajili ya matibabu ya magonjwa ya dharura, miundombinu kwa ajili ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU), na huduma ya afya ya mama na mtoto hasa eneo la upasuaji kuimarika.
Awali akitembelea hospitali hiyo alipata fursa ya kuingia wodi ya wazazi, wodi ya watoto, duka la dawa ,eneo la msamaha ambapo aliagiza ongezeko la ghorofa moja kutatua changamoto ya wagonjwa sita kukaa kitanda kimoja.
Akisoma taarifa Kwa Mh waziri Ummy, Mganga Mkuu wa hospitali hiyo amesema hospitali yake kwa ujumla inatoa huduma kwa wakazi 2,226,692, ambapo kwa siku inatoa huduma kwa wagonjwa wasiopungua 2500, na kulaza wagonjwa wasiopungua 70 kwa siku.
Awali akiongea na wagonjwa mbalimbali wanaopata huduma hospitalini hapo Mh Ummy amewashauri kujiunga na huduma za bima ya afya ili iwe rahisi kupata matibabu
Imetolewa na
Kitengo Cha Habari na uhusiano
Manispaa ya Kinondoni
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.