Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni yapongezwa kwa kasi nzuri ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kupitia mradi wa BOOST na SEQUIP ambayo ni matokeo ya usimamizi mzuri na shirikishi.
Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Deogratius Ndejembi (MB) leo tarehe 11 Julai, 2023 baada ya kutembelea baadhi miradi hiyo na kuridhishwa na kasi ya utekelezaji wake.
“Naipongeza sana Manispaa ya Kinondoni kwa utekelezaji mzuri wa miradi hii ya BOOST na SEQUIP kwani ukiangalia ujenzi huu umeanza kwa muda mfupi na sasa umefikia zaidi ya asilimia 95, kiukweli Kinondoni ni mfano wa kuigwa katika hili", amesema Mhe. Ndejembi.
Moja ya miradi iliyotembelewa na Mhe. Waziri ni ujenzi wa shule ya msingi Kunduchi na shule ya sekondari Kumbukumbu.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambule amemuahidi Naibu Waziri huyo kuwa Halmashauri itaendelea kusimamia kikamilifu miradi yote iliyoletwa na itakayoletwa na kuhakikisha inatekelezwa kwa kiwango kinachotakiwa na kukamilika kwa wakati.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini:
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.