NI BANDA LA KINONDONI PEKEE .
Nanaa ni aina ya mmea ambao asili yake ni Bara la Asia na huota kwa wingi Sana maeneo yenye baridi.
Kwa lugha ya kigeni hujulikana kama Mint.
JINSI YA KUOTESHA.
Baada ya kuandaa bustani yako kwa kuweka mbolea vizuri na kumwagilia, ukiwa taayari umeandaa vipande vya mche (cuttings) unaiotesha kwa kuichomeka kama matembele yanavyooteshwa kwa kuwa ni mmea unaotambaa sana. Na unapoiotesha lazima uzingatie mstari kwa mstari ni 60cm, na mche kwa mche ni 45cm.
Baada ya mwezi mmoja wa kuoteshwa, huwa inafaa kwa matumizi.
FAIDA ZAKE.
Mmea huu unafaida zifuatazo :
Ni mmea wenye Vitamini A, Ç na B6.
Huondoa maumivu ya tumbo.
Inasaidia kwa maswala ya mmeng'enyo wa chakula (Digestion).
Inatumika kutengeneza dawa ya Meno.
Husaidia kuondoa harufu mbaya ya mdomo.
Inatumika kama kiungo cha chai, au mboga yeyote.
Inaongeza damu.
Kupata haya na mengine mengi, usikose kutembelea banda la Manispaa ya Kinondoni kuelekea Nane nane Mkoani Morogoro na Kauli mbiu isemayo "Zalisha kwa tija mazao na bidhaa zitokanazo na Kilimo, mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa Kati ".
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.