Manispaa ya Kinondoni katika kutekeleza kauli mbiu ya maonesho ya wakulima, wavuvi na wafugaji inayosema "Wekeza katika kilimo, mifugo na uvuvi kwa Maendeleo ya viwanda " imeendelea kutoa elimu, utaalam, na ujuzi katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi katika kuhakikisha sera ya Uchumi wa Kati wa viwanda inatekelezeka.
Ukifika banda la Kinondoni kwa upande wa kilimo utakutana na wataalam watakaokufundisha kilimo cha mjini kitumiacho matumizi madogo ya eneo kwa kilimo cha faida chenye thamani, ulimaji mchicha lishe, kilimo cha biringanya, kilimo cha ngogwe, miembe, pilipili mbuzi, Nanaa bitruit, kabichi zambarau, kilimo cha uyoga, figiri na
Kadhalika kwa upande wa mifugo utakutana na mtaalam atakayekupatia elimu kuhusiana na utengenezaji wa malisho ya wanyama aina ya Azola na hydroponic fodder, utakutana na mtaalam atakayekuelezea matumizi sahihi ya ngozi za wanyama, ufugaji wa Ngombe chotara aina ya fresian, mbuzi aina ya Saanen, ufugaji wa kuku, Sungura, bata bukini, bata mzinga, kuku aina ya kuchi, simbilisi, Sungura na njiwa tausi.
Kwa upande wa uvuvi utakutana na mataalam atakayekupatia njia rahisi na sahihi kabisa ya kufuga samaki kitaalam na kuvua kwa faida kwa kutumia bwala la kisasa.
Lakini pia wajasiriamali waliowezeshwa utaalam na ushauri kutoka kwa wataalam wakionesha bidhaa zao za ujasiriamali walizozitengeneza kwa mikono yao.
Ni Kinondoni pekee kuelekea kilele cha maadhimisho ya nane nane Mkoani Morogoro, katika kutekeleza kauli mbiu isemayo "Wekeza katika kilimo, mifugo na uvuvi kwa Maendeleo ya viwanda "
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano na habari.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.