Timu ya Wataalam na Madiwani kutoka Halmashauri ya Kwimba Jijini Mwanza wamefanya ziara maalum ya mafunzo katika Manispaa ya Kinondoni kwa lengo la kujifunza namna ya uanzishaji na uendeshaji wa Shule za Msingi zinazotumia mchepuo wa lugha ya Kiingereza (English Medium). Ziara hiyo imefanyika Februari 26, 2024 ambapo
Wataalamu hao walipokelewa na Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Songoro Mnyonge, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Bi. Hanifa Suleiman Hamza, pamoja na Kaimu Afisa Elimu Msingi wa Manispaa ya Kinondoni.
Akiongea katika.ziara hiyo Mhe. Songoro aliwashauri wataalam hao kuwa sio lazima kuanza na Shule mpya, wanaweza kuchagua Shule moja wakaiboresha, wakaanza nayo kama ilivyo kwaanispaa ya Kinondoni ilivyofanya katika baadhi ya shule hizo.
"Kiuhalisia sio lazima kuanza na shule mpya hivyo mnaweza mkaanza na Wanafunzi wa darasa la kwanza huku hawa wengine wakiendelea, hamuwaondoi wanakuwa wanaondoka taratibu kwa kadri hawa wengine wanavyopanda darasa moja hadi lingine mwisho wa siku wanabaki Wanafunzi wa mfumo wa kiingereza pekee," amesema Mhe. Songoro.
Aidha Mhe. Songoro aliipongeza Halmashauri ya Kwimba kwa kufanya ziara katika Manispaa ya Kinondoni kwani ujio huo imeonesha Kinondoni kuna kitu lakini kuwa kioo kwa Halmashauri zote nchini katuka sekta ya elimu.
Kwa upande wao Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Tereza Lusangija pamoja na Mkurugenzi wa Halmashuri hiyo Bi. Happiness Msanga walishukuru na kufurahi sana kwa ushirikiano na mapokezi waliyoyapata kutoka Kinondoni.
Sambamba la hayo ziara hiyo ilikuwa mwanzo wa uhusiano mzuri kati ya Halmashauri ya Kwimba na Manispaa ya Kinondoni.
Wataalam na Maduwani hao walipata wasaa wa kutembelea Shule ya Msingi Oysterbay inayotumia mchepuo wa kiingereza na kupewa maelezo na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Egidius Mjunangoma.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.