Mstahiki Meya Manispaa ya Kinondoni Mhe. Songoro Mnyonge leo ameweka jiwe la msingi katika soko la Bwawani lililopo Kata ya Mwananyamala.
Akiweka jiwe hilo la msingi Meya Songoro amesema Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan iko mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wanapatiwa fursa za maeneo kwa ajili ya biashara ili waweze kujikwamua kiuchumi kwani ndio msingi endelevu wa ongezeko la kipato ngazi ya familia na Taifa kwa ujumla.
"Serikali ipo kwa ajili ya wananchi na hili soko la Bwawani ni kwaajili yenu wananchi, bidhaa zote zinapatikana hapa, hivyo mnakaribishwa kupata mahitaji yenu muhimu hapa, lakini pia mkinunua bidhaa mnawaunga mkono wafanyabishara wenzenu walioko hapa" Amesema Songoro.
Hafla hiyo imehudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Bi.Khanifa Suleiman Hamza, wafanyabiashara wa Soko la Bwawani pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.