Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mheshimiwa Songoro Mnyonge, amewataka wapangaji katika Stendi ya Mwenge kufungua fremu zao na kuanza biashara mara moja.
Mheshimiwa Songoro alitoa agizo hilo Juni 10, 2024 katika Kikao cha Robo ya Tatu cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri wa Manispaa ya Kinondoni kilichofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni.
Mheshimiwa Songoro alisisitiza kuwa Halmashauri imewekeza kwa kiasi kikubwa katika kuboresha miundombinu ya Stendi ya Mwenge ili kutoa fursa bora za biashara kwa wananchi. Aliongeza kuwa kufunguliwa kwa fremu hizo kutasaidia kuongeza mapato ya Halmashauri kupitia kodi na ushuru wa biashara, pamoja na kutoa ajira kwa wakazi wa eneo hilo.
Aliagiza kuwa, "Tumejenga Stendi ya Mwenge kwa gharama kubwa na tungependa Mwenge kiwe kituo Kikubwa cha biashara cha kuvutia ndani ya Manispaa ya Kinondoni. Tusingependa Mwenge iuawe badala ya kuwa kichocheo cha uchumi wa Wananchi wetu, pawe ni sehemu ya kukuza uchumi wa Wananchi wetu na hayo ndiyo matarajio yetu. Hivyo basi wote waliopewa fremu pale katika Stendi ya Mwenge waende wakafungue biashara na wafanye biashara mara moja."
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.