Jamii imetakiwa kuepukana na migororo ya kifamilia ambayo ndiyo chanzo kikubwa cha watoto kuingia mitaani na kufanyiwa vitendo vya kikatili.
Hayo yameelezwa Machi 21, 2024 na Afisa Ustawi wa Jamii wa Manispaa ya Kinondoni, Bi. Struda Nselu, katika kikao kilichowakutanisha walezi wa watoto waliotokea katika mazingira magumu kwa lengo la kufanya tathmini na changamoto wanazopitia katika malezi ya watoto hao.
"Naomba famili zisiingie kwenye migogoro kwani migogoro ndio sababu ya watoto kuingia mitaani na kufanyiwa ukatili."Kwa upande wake Mdau kutoka Shirika la Global Child Advocates Tanzania, Bw.Francis Mwakatenya, ameitaka jamii kuhakikisha watoto wanalelewa katika mazingira ya ndani ya familia ili kuwajenga kimaadili.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.