Elimu hiyo imetolewa leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya ofisi ya Afisa mtendaji Sinza ukiwahusisha wananchi wa Sinza A, B, C, D na E ambao ndio walengwa mahususi wa mradi.
Katika mkutano huo wa hadhara ilielezwa kuwa Lengo kuu ni kuutambulisha mradi na kutoa elimu na ushauri utakaoweka Mazingira rafiki yatakayowezesha utekelezwaji wake, kwa kuzingatia weledi, ufanisi na ubora uliokusudiwa.
Akiambatana na timu ya wasimamizi wa mradi huo, Bi. Pendo Fred, ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Kinondoni amesema, ni vema kuundwa kamati za watu watano kila mtaa kwa lengo la kutoa taarifa stahiki kuhusiana na mradi mzima ikihusisha faida zitakazopatikana wakati na baada ya mradi kukamilika, kwani hiyo ndiyo njia sahihi itakayomwezesha mwananchi yeyote kutoa ushirikiano pale inapobidi, na pia kujua nini wajibu wake na namna ya kutoa taarifa ikiwa kutakuwa na shida yoyote inayoweza kuzalishwa na mradi wakati wa utekelezaji.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Sinza Mhe Godfrey Chikandamwali amewashukuru na kuwaahidi wasimamizi wa mradi huo kuendelea kuwaunga mkono kwa kuwa miradi yote ni kwa faida ya wananchi na kusema jukumu walilofuata katika mkutano huo ni jema.
Mradi huo utahusisha barabara ya Shekilango mpaka Bamaga awamu ya saba kwa urefu wa km 3.7 kwa usimamizi wa kampuni ya China Road and Bridge Corporation ambao tayari ulishaanza kutekelezwa tangu July 2019, na utakamilika Octoba 2019.
Imeandaliwa na
Kitngo cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.