Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kupitia Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe imetoa mafunzo na ushauri wa lishe sambamba na huduma jumuishi za afya ikiwemo upimaji wa presha, upimaji wa kisukari, upimaji wa hali ya lishe kwa watoto chini ya miaka 10 pamoja na kuwapa dawa za vitamini C na uchangiaji damu.
Mafunzo hayo yamefanyika katika Kata ya Mikocheni Oktoba 7,2023.
Katika mafunzo hayo msimamizi wa magonjwa yasiyoambukiza kutoka Manispaa ya Kinondoni Dkt.Omary Mwangaza amewataka wananchi kuzingatia makundi matano ya chakula ili kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza.
Aidha Dkt. Mwangaza amewashauri wananchi kupima afya zao ili kujua namba za wagonjwa hasa kwa magonjwa yasiyoambukiza kwani magonjwa hayo yamekua ndio chanzo cha vifo vya mapema.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.