Elimu ya Kilimo Mjini ni muhimu katika kukuza uzalishaji na utunzaji wa mazingira na matumizi mazuri ya ardhi mijini.
Akiongea katika maadhimisho ya NANE NANE yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. Nyerere mkoani Morogoro Bw. James Mtambalike anajishughulisha na Kilimo Mjini amesema, lengo la kuanzisha kilimo hiki ni baada ya kutambua kuwa ni kilimo chenye tija kwa kuwa linatumika eneo dogo kwa manufaa makubwa.
Bw. Mtambalike amesema Kilimo Mjini kimempa manufaa makubwa ikiwemo kupata kipato, kuwa na mtandao mkubwa uliompelekea kuongeza elimu kuhusiana na kilimo na ujasiriamali kwa ujumla.
Aidha," Kilimo Mjini hakihitaji eneo kubwa unaweza tumia mifuko au makopo kwa kupanda maua, mboga mboga na mazao mengine". Amesema.
Utunzaji wa Kilimo Mjini hauna ugumu wowote, mkulima anaweza kuzalisha mazao sehemu yoyote ikiwemo kwenye makazi ya kuishi.
Vile vile amesisitiza jamii ijifunze kuhusiana na Kilimo Mjini kwani ni rahisi, masoko yanapatikana kirahisi ambayo ni maeneo ya sokoni na supermarket.
Amesisitiza kuwa maonesho ya Nane Nane yamesaidia jamii kupata elimu kuhusu Kilimo Mjini na kupelekea kuongezeka kwa uzalishaji. "Wadau wanaendelea kupokea elimu ya kilimo hiki na kutoa mrejesho wa mazao wanayozalisha". Amesisitiza Mtambalike.
Matarajio ya mkulima huyu ni kuendelea kutoa elimu kupitia mikoa mbalimbali ili jamii iendelee kupata uelewa zaidi juu ya kilimo hiki.
Kauli mbiu ya maonesho haya ni "Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula".
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini:
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.