Utoaji wa elimu kwa jamii na utunzaji mazingira vimetajwa kuwa vichochezi vya kupunguza maafa na athari za majanga katika jamii.
Hayo yamesemwa na Mratibu wa Maafa, Manispaa ya Kinondoni, Bi. Pendo Fredy Mwaisaka, wakati akielezea juhudi zinazotekelezwa na Manispaa katika kukabiliana na maafa kwa washiriki wa semina ya kujenga uelewa wa upunguzaji madhara ya maafa katika jamii.
Semina hiyo, inaendeshwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Uhamaji (IOM).
Mratibu huyo alizataja Kata 13 zinaongoza kwa maafa yatokanayo na mafuriko Wilaya ya Kinondoni kuwa ni pamoja na Kigogo, Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni, Kunduchi, Mbweni, Mbezi Juu, na Msasani. Kata nyingine Ni Bunju, Tandale, Mzimuni, Makumbusho na Kawe. Sababu zinazochangia maafa ni pamoja na ujenzi holela, mabadiliko ya hali ya hewa, maporomoko ya udongo, uharibifu wa mazingira na kuziba mifereji inayotirirsha maji ya mvua.
"Tunajitahidi kutoa elimu kwa jamii ya utunzaji wa mazingira lakini pia wajenge kwa kufuata taratibu za mipangomiji. Aidha DMDP imetekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa mifereji mikubwa na ujenzi wa mto ng'ombe ili kukabiliana na maafa," alisema Bi. Mwaisaka.
Semina hiyo ya siku mbili imeanza kwa kushishirikisha washiriki kutoka Kata 13 Kati ya 20 za Manispaa ya Kinondoni ambayo pia imehudhuriwa na Mwakilishi wa IOM, Waratibu wa Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambao kwa pamoja wameeleza umuhimu wa jamii kuwa tayari kukabiliana na maafa.
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini: Manispaa ya Kinondoni
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.