Ni rai yake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Alli Hapi, alipokuwa akijibu hoja za wananchi zilizoletwa kwake katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kinondoni shamba, Manispaa ya Kinondoni.
Amesema wananchi wengi hukosa huduma za msingi kwa wakati kwa kile kinachodaiwa kutokuwa na elimu nacho, hali inayopelekea kujenga matabaka yenye taswira hasi za mgawanyo wa huduma katika jamii.
"Serikali yetu ni ya haki na usawa katika nyanja zote, na elimu ndio nguzo imara ya kuelekea kwenye haki yako, sasa kama mwananchi hana elimu ya huduma zinazoendelea, atapataje huduma, toeni elimu kwa wananchi hawa, ili waweze kuwa na ufahamu wa huduma na fursa zinazopatikana kwenye Halmashauri yao " Ameongeza Hapi
Akitolea ufafanuzi kuhusiana na mikopo ya wanawake na vijana, Bi Florah Msilu ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii ,amesema mikopo ya wanawake na vijana ni utekelezaji wa program ya Serikali kufuatia agizo la mwaka 1998, linaloitaka Halmashauri kutenga asilimia kumi ya mapato yake ya ndani kwa lengo hilo.
Amesema kwa Kata ya Kinondoni hadi kufika leo kiasi cha tsh milioni 85,094,000/=zimekwishatolewa, kwa vikundi 21 vilivyotoka mitaa ya kumbukumbu, Kinondoni mjini, Kinondoni shamba, na Ada Estate.
Bi Florah ameongeza kuwa Mikopo hiyo ni haki ya kila kijana au mwananmke yeyote aliyejiunga katika kikundi cha watu watano na kukamilisha taratibu zote zikiwemo usajili.
Akifunga mkutano wake wa hadhara katika Kata ya Kinondoni Mkuu huyo wa Wilaya amesisitiza utekelezaji wa maagizo yake yakiwemo mgambo kuacha kupiga na kunyanyasa wananchi, Malipo yote halali yatolewe risiti za mashine, watendaji wa kata shirikianeni na wananchi kudhibiti uchafu, Kuwepo na vibebea uchafu kwenye Kata na Mitaa ya maeneo tunakoishi, pamoja na kufanya kazi kwa haki na wajibu katika kuiletea nchi yetu matokeo chanya ya utekelezaji wa sera, mipango na mikakati kuelekea uchumi wa kati wa viwanda.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano na habari.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.