Imeelezwa kuwa Mfumo wa Mawasiliano wa e-Board utarahisisha mawasiliano na utunzaji wa nyaraka muhimu za vikao vya Madiwani.
Hayo yameelezwa leo Desemba 4, 2023 na Mstahik Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mheshimiwa Songoro Mnyonge, wakati akifungua mafunzo ya mfumo wa TEHAMA (e-Board) kwa Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni.
Alisema, "mafunzo haya yatarahisisha mawasiliano, kupunguza gharama za karatasi, kuokoa muda na taarifa mbalimbali kuwafikia haraka."
Mfumo huu wa kidigitali unawezesha sekretarieti kuandaa yatokanayo kwenye kikao, wajumbe kupiga kura na kuwawezesha wajumbe wa menejimenti kutengeneza ripoti za utendaji kazi katika vipindi mbalimbali vya mwaka.
Aidha, Afisa TEHAMA Bw. Jones Njelekela ameongeza kuwa, mafunzo haya yatarahisisha mawasiliano baina ya Madiwani, itapunguza gharama, itaokoa muda sambamba na kubadilishana taarifa zitakazotakiwa kuwafikia kwa wakati.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.