*Aonya Watumishi Kushiriki Magendo
Watumishi wa Manispaa ya Kinondoni wameonywa kutojihusisha na biashara za magendo ili kulinda hadhi na hatma ya utumishi wao.
Tahadhari hiyo, ni moja ya maelekezo 22 yaliyotolewa Machi 27, 2024 na Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Toba Nguvila, wakati akiongea na watumishi wa Manispaa hiyo katika ukumbi wa Sekondari ya Turiani.
Dkt. Nguvila alisema, "Nimeagizwa na Mkuu wa Mkoa kuwatahadarisha watumishi kutojihusisha na magendo. Utahatarisha ajira yako na ni fedheha kwa viongozi wako." Alionya upitishwaji wa bidhaa za magendo kwa kuhoji, " iweje magendo yapite wakati viongozi wa Mitaa na Kata mpo sehemu hizo?"
Katika kikao hicho kilicho wahusisha Watendajimwa Kata, Watendaji wa Mitaa, Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Idara na watumishi kutoka Makao Makuu ya Manispaa, Dkt. Nguvila pia alitoa maelekezo mengine 21 ambayo ni pamoja na kuhamasisha wananchi wanao ishi mabondeni kuhama mara moja, ulinzi wa watoto dhidi ya unyanyasaji, ujenzi wa vyuo vya ufundi, kubuni vyanzo vipya vya mapato, kuzuia uvujaji wa mapato na kumaliza kero za ardhi haswa eneo la Mabwepande.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.