Wajasiriamali wadogowadogo zaidi ya 200 Kata ya Mzimuni wamewezeshwa kwa kupewa bidhaa mbalimbali ili kubusti mitaji ya biashara wanazofanya.
Hafla hiyo iliyoandaliwa na Diwani wa Kata ya Mzimuni Mhe. Manfred Lyoto imefanyika Mei 22, 2024 katika Ofisi ya Kata ya Mzimuni ikiwa na lengo la kukuza mitaji ya wajasiriamali hao katika shughuli zao za ujasiriamali.
Wajasiriamali hao wamepatiwa bidhaa hizo kutokana na shughuli wanazozifanya kwa kila mjasiriamali, bidhaa zilizotolewa ni pamoja na sukari, mafuta ya kupikia na unga wa ngano.
Kwa upande wake, Mtendaji wa Kata hiyo ndg. Mickdad Ngatumbura amewataka wajasiliamali hao kutumia bidhaa hizo kwa lengo lililokusudiwa ili wazidi kuimalisha shughuli zao na kukua zaidi kiuchumi.
"Sambamba na bidhaa hizi zilizotolewa niwaombe na kusisitiza mkatumie kama vile ilivyokusudiwa na siyo vinginevyo." Ameongeza Ndg. Mickdad.
Kadhalika, Mtendaji huyo amegusia suala la mikopo ambapo amesema Serikali inaendelea na mkakati wa mikopo ya asilimia kumi hivyo amewataka wajasiliamali kutumia fursa hiyo na kuhakikisha wanarudisha mikopo hiyo kwa wakati ili kunufaika kwa mara nyingine ya kupata mikopo hiyo.
Ndg. Ngatumbura ameendela kuwasisitiza wajasiliamali hao kuhakikisha wanafuata kanununi za kuwa na kitambulisho cha ujasiliamali ili kuepukana na usumbufu wanapokua katika biashara zao.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.