Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Bi. Hanifa Hamza amefungua rasmi dirisha la utoaji wa mikopo ya asilimia kumi kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu Oktoba 1, 2024.
Akizungumza wakati wa ufunguzi huo uliofanyika katika Kikao cha Mafunzo ya utoaji mikopo kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii, Bi. Hanifa aliwaasa Maafisa Maendeleo ya Jamii kutekeleza majukumu kwa uadilifu kwa kutoa mikopo kwa vikundi vinavyostahili.
"Maafisa Maendeleo mnapaswa kufuata taratibu zote za utoaji mikopo kwa uadilifu mkubwa. Ni lazima tuhakikishe kwamba kila kikundi kinachopokea mikopo hii kina sifa stahiki, na fedha hizi zinawafikia walengwa sahihi," alisema.
Katika hatua nyingine, Maafisa Maendeleo walipewa jukumu la kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024.
"Pia hakikisheni mnatoa elimu ya kujiandikisha na kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024 kwa wanavikundi wote watakaokuja kuchukua mikopo." Alisema.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.