Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Saad Mtambule amezindua Mradi wa ujenzi wa bomba la uchakataji maji taka wenye thamani ya bilioni 124 ambao utaunganisha zaidi ya Kaya 11,000 bure ili kuweka mazingira safi na salama. Uzinduzi huo umefanyika Mei, 24, 2024 katika Kata ya Mbezi juu ambapo Mhe. Mtambule amewataka viongozi kusimamia mradi huo na kuhamasisha wananchi kushiriki ipasavyo.
"Ujio na utekelezaji wa mradi huu una faida na maslahi mapana kwa Wananchi wa Kinondoni hivyo kila mmoja anapaswa kujisajili na kuhakikisha anaingia katika mradi huu kwani mradi huu ni bure na ni wajibu kwa kila Mwananchi kushiriki". Amesema, Mhe. Mtambule.
Mhe. Mtambule amesisitiza kulinda Miundombinu na kuhakikisha hatua za kisheria zinachukuliwa kwa uharibufu wa miundombinu utakaojitikeza. Pia, Mkuu wa Wilaya huyo amewataka viongozi kuanzisha Kampeni ya mguu kwa mguu ambayo itasimamia ipasavyo kasi ya ujenzi wa mradi huo na kukamilika kwa wakati. Aidha, Mhe. Mtambule ameeleza faida za mradi huo ni pamoja kupunguza kero ya maji taka kwenye makazi ya watu, kuondokana na tatizo la magonjwa ya milipuko, kuweka mazingira safi na salama pamoja na kupunguza gharama za unyonyaji majitaka kwa wananchi.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.