Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mheshimiwa Saad Mtambule, Juni 21, 2024 ametoa Bima za Afya kwa walemavu wa Macho waliopo eneo Kituo cha Afya Manyanya Kata ya Kinondoni. Lengo ni kuboresha na kuimarisha huduma ya afya nchini.
Alisema, "Ulemavu sio kikwazo cha kuwa tegemezi hivyo niwaombe tuendelee kuchapa kazi kama ambavyo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akihimiza Wananchi kuchapa kazi ili kuleta maendeleo ndani ya Taifa letu."
Aidha, Mheshimiwa Saad aliwataka watu wote waliopatiwa Bima hizo kuzitumia kama ilipangwa kwani Serikali imekuwa ikiguswa sana na afya za watu wenye uoni hafifu.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.