Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Alli Hapi ametoa siku ishirini na moja (21), kwa wakala wa barabara Mijini na Vijijini (TARURA) kuanza matengenezo ya urefu wa Km 1 kati ya Km 3.45 za urefu wa barabara ya African Kinzudi iliyoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha.
Amelitoa agizo hilo leo alipokuwa katika ziara yake ya ukaguzi wa barabara ambapo alifanikiwa kutembelea barabara hiyo ya Africana Kinzudi na kujionea hali halisi ya uharibifu uliotokea na kusababisha adha kubwa kwa wananchi hasa waenda kwa miguu.
Amesema kiwango cha maji kinachoshuka kwenye barabara hiyo ni cubic meter 11 kwa sekunde ,hivyo ni maji mengi ikilinganishwa na uwezo wa barabara wenyewe kuhimili kiwango hicho.
"Nimejionea mwenyewe namna gani maji yanavyoshuka kutoka kule juu yanavyosababisha uharibifu mkubwa wa barabara na wananchi wangu wanavyopata shida, ........nataka niwahakikishie wananchi wangu wote ambao wanakumbwa na adha ya barabara hii ndani ya wiki tatu kutoka hivi sasa tutaanza kutengeneza km moja ya barabara hii...... na kazi hii itafanywa na wakala wa barabara za mijini na vijijjini TARURA." Ameagiza Hapi.
Katika hatua nyingine ametoa siku 14 kwa wananchi walioingia katika hifadhi ya barabara kubomoa mara moja majengo yao kupisha matengenezo ya barabara hiyo yanayotarajia kuanza mapema.
Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.