NI KWA WALE WANANCHI WANAOKAA KARIBU NA BONDE KWA MADAI YA KUSAIDIWA MWANASHERIA WA KUWATETEA KUTOBOMOLEWA NYUMBA ZAO.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Alli Hapi ametoa masaa 72 kwa wananchi wa kigogo kurudishiwa fedha walizokuwa wakichangishwa kwa madai ya kusaidiwa kutobomolewa nyumba zao.
Ameitoa kauli hiyo leo alipokuwa akiongea na wananchi wa Kigogo katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la lililokuwa dampo ya zamani.
Amesema ukusanyaji huo wa fedha hizo ni wizi na unawaletea wananchi hofu kitu ambacho sio mpango wa Serikali ya awamu ya tano, na pia ni kutaka kuwanyonya wananchi wanaofanya kazi zoa.
"Taarifa hizi ninazo muda mwingi, nilikuwa natafuta timing nzuri ya kulizungumnza, nawapa masaa sabini na mawili kutoka sasa, fedha zote walizokusanya kwa kinamama, kwa wazee, nyumba kwa nyumba ya kuwadanganya watu kwamba watawatafutia mtu wa kuwatetea wasibomolewe wakati mtu huyo wa kuwatetea ni sisi Serikali ,watu hawa nawapa masaa sabini na mbili warudishe fedha zote, huo ni wizi kama wizi mwingine wa wananchi " Ameagiza Hapi.
Aidha amemtaka OCD wa Wilaya ya Magomeni kuhakikisha anapata taarifa ya maandishi kutoka kwa Kaimu Mtendaji wa kata ya Kigogo Bi.Sarah Mwinuka ya kuwa nani amerudisha fedha au hajarudisha fedha.
"Baada ya masaa hayo, OCD nataka watu wote wakamatwe, hata kama kunamwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, na wakisharudisha hizo fedha, waniandikie barua ya kuomba radhi kwa kosa walilolifanya. "Amesisitiza Hapi.
Amewataka wananchi kutokuwa wepesi kudanganywa na matapeli, kwani fedha yeyote inayokusanywa lazima iwe na tarifa na lazima ifuate taratibu zote za kifedha za Nchi ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano na Habari
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.