Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Saad Mtambule ameitaka Bodi ya Michezo ya kubahatisha kusimamia Sheria za Michezo ya Kubahatisha.
Mheshimiwa Mtambule aliyasema hayo Oktoba 3, 2024 katika Semina kwa Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi iliyofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni yenye lengo la kutoa elimu kuhusiana na michezo hiyo.
Mhe. Mtambule alisisitiza kutekelezwa Kwa Sheria za Michezo hiyo kwa kuhakikisha mashine zinasajiliwa na kupata leseni.
Aliagiza kuondolewa haraka kwa mashine katika maeneo yasiyo na kibali kabla ya kuchukuliwa hatua.
Pia, alisisitiza kufanyika kwa uratibu, usimamiaji, ufuatiliaji na ukaguzi wa michezo hiyo mara kwa mara ili kuhakiksha michezo inafuata taratibu na kuendelea kuongeza mapato katika Wilaya yetu.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.