NI WALE WASIOFANYA KAZI ZAO KWA WELEDI, HALI INAYOPELEKEA UCHELEWESHWAJI WA UKAMILISHAJI WA MIRADI YA MAENDELEO.
Kauli hiyo imetolewa leo, na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Daniel Chongolo katika ziara yake ya ukaguzi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kujiridhisha na hatua za utekelezaji zilizofikiwa.
Amesema wakandarasi ni lazima waelewe umuhimu wa kutekeleza na kukamilisha miradi hii kwa mujibu wa makubaliano na mikataba waliyoingia kwani kwa kutokufanya hivyo kunarudisha nyuma maendeleo na ni kutoitendea haki si tu Serikali bali hata wananchi walengwa wa mradi unaotekelezwa.
Aidha Mhe. Chongolo ameonesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata taka kinachojengwa na mkandarasi wa Kampuni ya CRJE East Africa LTD kwani katika kipindi Cha miezi 11 ya mkataba wake mradi huo umekamilika kwa asilimia 20 pekee na huku akiwa amebakiwa na miezi 7 ya kumaliza mkataba.
Amesema "wakandarasi Kama hao hawatavumiliwa katika Wilaya yangu na endapo itafika tarehe 30 mwezi June bila kuonesha dalili za mabadiliko ya mradi huo mkandarasi huyu achukuliwe hatua sitahiki.", Mh. Chongolo.
Kadhalika amekemea tabia ya baadhi ya wakandarasi wakubwa kuchukua tenda za Ujenzi na baadae kuwapa kandarasi wengine au wadogo kuifanya kazi hiyo, huku wao wakibaki kuwa kama madalali.
Katika hatua nyingine amewataka watendaji wa Kata kusimamia kwa ukaribu miradi hiyo ili iweze kukamilika kwa wakati na iweze kuleta tija kwa jamii
Miradi iliyotembelewa na Mkuu wa wilaya leo ni pamoja na Barabara ya Tegeta nyuki, Barabara ya Boko Magereza, Hospitali ya Wilaya ya Mabwepande, Shule ya wasichana ya Mabwe Tumaini girls, Kiwanda cha kuchakata taka kilichopo Mabwepande na Shule ya wavulana ya Mbweni Teta.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.