NI ILE INAYOTEKELEZWA KWA USHIRIKIANO KATI YA SERIKALI YA TANZANIA NA INDIA INAYOHUSISHA MATANKI YA MAJI PAMOJA NA BUSTA .
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Alli Hapi amefanya ziara kutembelea miradi ya maji inayotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na India iliyogharimu takribani bilioni 80.
Ziara hiyo imefanyika leo katika maeneo ya Changanyikeni, Bunju, Salasala Makongo, Goba na Mabwepande ambapo Mkuu huyo wa Wilaya amepata fursa ya kukagua hatua za utekelezaji wa mradi ulikofikia pamoja na kiwango cha ubora ilichonacho miradi hiyo.
Akiongea mara baada ya ukaguzi Mh Hapi amesema miradi hiyo Mara itakapokamilika itapunguza tatizo la maji katika Wilaya yake kwa asilimia 95 huku wanufaika wakubwa wakiwa wakazi wa maeneo husika.
Amesema Serikali ya awamu ya tano inalo lengo dhahiri la kuhakikisha inawaondolea wananchi wake kadhia ya tatizo sugu la maji na ndio maana kwa kushirikiana na India inatekeleza mpango huo mkubwa wa mradi wa maji kwa Wilaya ya Kinondoni.
Aidha amewataka makandarasi wanaoendelea na ujenzi wa miradi hiyo ya maji kuhakikisha wanakamilisha ujenzi huo kwa ubora na kwa wakati ili wananchi waweze kunufaika na huduma hiyo ya Maji.
"Nitoe wito kwa makandarasi Hawa kufanya Kazi usiku na mchana ili kuhakikisha miradi hii inakamilika kwa wakati, na sisi Kama Serikali tupo tayari kutoa ulinzi kama wao wataonesha utayari wa kafanya Kazi usiku na mchana" Amesema Hapi.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa huduma za ufundi toka DAWASA Bi Modester Mushi amesema miradi hii ya maji inatokana na kukamilika kwa upanuzi wa mradi mkubwa wa wa maji wa Ruvu chini na kwa Wilaya ya Kinondoni utahudumia zaidi ya wakazi laki Moja na sitini.
Miradi hii inayoendelea kujengwa inatarajiwa kukamilika mwezi February mwaka huu na kukadiriwa kupunguza tatizo la maji katika Wilaya ya Kinondoni kwa asilimia 95.
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano na Habari
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.