NI ZILE ZINAZOTEKELEZWA NA WAKALA WA BARABARA MIJINI NA VIJIJINI (TARURA) PAMOJA NA ZILE ZILIZOKO CHINI YA MRADI WA DMDP.
MKuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Alli Hapi amefanya ziara kukagua hatua zilizofikiwa za utekelezaji wa miradi ya barabara zinazotekelezwa na wakala wa barabara mijini na vijijini (TARURA) pamoja na zile zilizoko chini ya mradi wa DMDP zenye thamani ya takribani bilioni 18
Akikagua barabara hizo Hapi amesema ni kufuatia kuharibika kwake kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha, hali inayoleta usumbufu na athari kubwa kwa wananchi hasa wale watembea kwa miguu.
Ameongeza kuwa athari nyingi za kuharibika kwa barabara hizi husababishwa na wananchi kujenga kwenye hifadhi ya barabara na kuziba mikondo ya maji kunakopelekea mafuriko na hivyo kuwataka wabomoe wenyewe.
"Leo nimetembelea miradi ipatayo mitatu ya barabara yenye thamani ya takribani bilioni 18"Amebainisha Hapi.
Kadhalika amezitaja barabara hizo kuwa ni barabara ya Makanya eneo la daraja la Uzuri, barabara ya Makongo Goba pamoja na Ile ya Africana Salasala Kinzudi.
Katika hatua nyingine Maneja wa TARURA Manispaa ya Kinondoni Ndg Leopod Rungi amesema wamejipanga kuhakikisha barabara zinazohitaji matengenezo kufanyika kwa wakati na kwa kiwango cha ubora uliokusudiwa.
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano na Habari
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.