Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ali Hapi ametembelea kiwanda cha kuzalisha mayai na kutotolesha vifaranga cha AKM Glitters kilichopo Mbezi Wilaya ya Kinondoni.
Katika ziara yake aliyoambatana na kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya hiyo alionesha kufurahishwa pale alipokuwa akipatiwa taarifa ya kiwanda hicho kuhusiana na uzalishaji na uendeshaji wake.
Amesema viwanda hivi ni fursa kwa vijana wasio na ajira, na hasa ikizingatiwa Serikali ya awamu ya tano ni Serikali ya viwanda.
Ameongeza kuwa ipo haja ya kuhakikisha viwanda hivi vinatambuliwa ili viweze kupatiwa elimu na utaalamu unaotakiwa kutoka kwa wataalam wetu wa Mifugo wa Manaispaa.
Akielezea kuhusu shughuli za kiwandani hapo Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bi Elizabeth swai amesema kiwanda kinajishughulisha na ufugaji wa Kuku aina ya Kuroiler, kinatotolesha vifaranga na kinao uwezo wa kutotolesha mayai elfu sitini kila baada ya siku ishirini na moja (21) kwa kutumia mashine za kitaalamu (incubators).
Ameongeza kuwa kiwanda hicho pia kinajishughulisha na utengenezaji wa chakula cha kuku, pamoja na ufugaji wa Kuku hao.
Kiwanda kimekuwa na uwezo wa kutoa ajira kwa vijana zaidi ya themanini (80) wa hapa hapa nchini Tanzania.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.