Kamati ya Afya ya Msingi Manispaa ya Kinondoni imefanya kikao leo kujadili juu ya kampeni ya utoaji wa chanjo ya matone ya Polio awamu ya tatu kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.
Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Godwin Gondwe amewasisitiza wazazi na walezi kuwapa ushirikiano wataalamu wa afya kwa kuwatoa watoto wao waweze kupata chanjo ya matone ya Polio ili kuwakinga na ugonjwa wa kupooza(POLIO).
Gondwe amesema Manispaa ya Kinondoni inatarajia kuwafikia watoto walio chini ya umri wa miaka mitano wapatao 223,541 kwa muda wa siku nne za kampeni kuanzia tarehe 1 hadi 4 Septemba, 2022.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Bi. Hanifa Suleiman Hamza, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dkt. Samwel Laizer, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, pamoja na baadhi ya watumishi wa Manispaa.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.