Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Godwin Gondwe amewataka wadau wote ufukwe wa Coco beach kuimarisha ulinzi na usalama na kukomesha kabisa vitendo vya ubakaji na udhalilishaji katika eneo hilo.
Hayo ameyasema wakati akizungumza na wafanyabiashara, waokoaji, wawekezaji na wadau wengine wanaohusika na ufukwe wa Coco beach wakiwemo viongozi na watendaji wa Chama na Serikali kuanzia ngazi ya Mtaa hadi Wilaya.
Mheshimiwa Gondwe pia ametoa maelekezo yatakayowezesha kuimarisha ulinzi na usalama na kuifanya Coco beach kuwa mahali salama kwa watumiaji ikiwa ni pamoja na kusajili maboya yote na wamiliki wake, kuweka katika rekodi kila mteja anayekwenda kuogelea na mtu aliyeondoka naye na kuwabaini wageni wote wanaokuja na kuondoka siku za Jumamosi na Jumapili na kufanya uhalifu.
Pia amewaagiza Maafisa Maendeleo ya Jamii kuhakikisha wanawake na vijana wanaofanya biashara katika eneo hilo kuhakikisha wanaundiwa vikundi vya mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu inayotolewa na Manispaa.
Mwisho amewashukuru viongozi mbalimbali wanaofanya jitihada kubwa kuhakikisha eneo la ufukwe wa Coco beach linaboreshwa na kuwa katika viwango vya kimataifa ambapo alimtaja Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Amos Makalla, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa na viongozi wengine wa Chama na Serikali na kuahidi kuunga mkono kwa vitendo jitihada za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuimarisha utalii nchini.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.