Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Godwin Gondwe leo Jumanne tarehe 19 Oktoba, 2022 amefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi mitatu ya maendeleo ya soko la Msasani, stendi ya mabasi Mwenge na uwanja wa mpira wa miguu wa timu ya KMC FC uliopo Mwenge Kata ya Kijitonyama.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ameridhishwa na hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa miradi hiyo na kuagiza kuondoa changamoto zote zilizopo kwa kushirikisha wadau wote muhimu wa miradi hiyo ili ikamilike kwa wakati na kuwanuifaisha walengwa wa miradi hiyo.
Katika mradi wa soko la Msasani linalojengwa kwa fedha za Kitanzania shilingi milioni 286 Mhe. Mkuu wa Wilaya amemwagiza Mhandisi wa Manispaa kufanya kikao cha pamoja na wadau wote wa ujenzi wa soko hilo na watumiaji wake na kuandaa mchoro wa maeneo yatakayotumiwa na wafanyabiashara za chakula mama lishe ili liweze kutosheleza wafanyabiashara wote 24 waliopo sokoni hapo.
Aidha ametoa maelekezo ya kuhakikisha mradi huo unakamilika ndani ya siku 30 kwa sababu fedha zote za kuwezesha kukamilisha mradi ziko katika akaunti ya Kata ya Msasani.
Akizungumzia miradi ya ujenzi wa stendi ya mabasi na kiwanja cha mpira wa miguu cha KMC FC kilichopo Mwenge, amewataka Wakandarasi wakamilishe miradi hiyo ndani ya muda uliopangwa ili Halmashauri iweze kuanza kunufaika kwa kukusanya mapato yatakayowezesha kutekeleza miradi mingine ya maendeleo.
Wahandisi washauri na Wakandarasi wa miradi hiyo wamemhakikishia Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Gondwin Gondwe azma ya kukamilisha miradi hiyo kwa wakati ifikapo Februari 3 mwaka ujao 2023 ambapo ameahidi kuja kujiridhisha baada ya muda huo.
Miradi yote mitatu iliyotembelewa ina thamani ya zaidi ya shilingi za Kitanzania bilioni kumi ambapo wadau wote walimshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassani na Serikali kwa ujumla kwa kutekeleza miradi hiyo muhimu na yenye manufaa kwa wananchi wote.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini:
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.