Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imepokea vifaa vya kunawia mikono (zaidi ya ndoo 100) pamoja na Vitakasa mikono kutoka mtandao wa kubashiri wa SportPesa kwa lengo la kuwasaidia wananchi kujikinga na maambukizi ya homa ya mapafu inayosababishwa na Virusi vya COVID 19 (Corona).
Vifaa hivyo vya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona vimepokelewa na Mkuu wa Wilaa hiyo Mhe. Daniel Chongolo ,akiwa ameambatana na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Dk. Patricia Henjewele, Mganga Mkuu Samweli Laizre pamoja na Katibu Tawala Bi Stella Msofe.
Akizungumza wakati wakupokea vifaa hivyo, Mhe. Chongolo amesema kuwa Kinondoni imepokea vifaa hivvyo na kwamba wataendelea kuhamasisha wadau wengine waweze kuchangia ili kuendelea kudhibiti ugonjwa huo usisambae kwenye maeneo mengine.
Amefafanua kuwa Virusi vya Corona vimekuwa janga kubwa Duniani na kwamba Wilaya hiyo imejipanga kuhakikisha kuwa kila mmoja anatumia vitakasa hivyo ili kujikinga na maambukizi ya Virusi hivyo pasipo kuambukiza wengine.
“Kama mkuu wa Wilaya ninashukuru kwa msaada huu, kwetu utasaidia kwa sababu ofisi zote za Serikali za mitaa na Kata zitapata seti za vifaa hivi, tutakuwa huru kwa kuendelea kutoa huduma kwa wananchi kama kawaida, ndio mana mmeona hapa kila anaeingia ana nawamikono yake kabla ya kuingia kupatiwa huduma” amesema Mhe. Chongolo.
Mhe. Chongolo ameongeza” kwetu sisi hatupambani kama Kinondoni, tunapambana kama mkoa ,nandio jukumu tulilopewa , hivyo hivyo nitumie fursa hii kuwaalika wadau wengine wenye mapenzi mema kutupatia vifaa vingine.
Mhe. Chongolo ameeleza kuwa Wilaya hiyo imejipanga vizuri katika kupambana na virusi vya Corona ikiwemo kuendelea kutoa matangazo ya kuhamasisha na kuelimisha wananchi namna ya kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo.
Kwaupande wake Mkurugenzi wa uendeshaji kampuni ya SportPesa nchini, Abbas Tarimba, amesema kuwa ndoo hizo zakunawia mikono zitasaidia wananchi ikiwa ni hatua ya kujikinga na virusi hivyo vya homa ya mapafu inayosababishwa na Covid 19.
Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.