Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo leo amefanya ziara katika soko la Tandale na Magomeni kwa lengo la kuangalia maendeleo ya ujenzi na kusikiliza maoni mbalimbali waliyonayo wafanyabishara hao kuhusiana na ujenzi unaoendelea.
Mhe. Chongolo amesema kuwa ameridhishwa na namna hatua ya ujenzi wa masoko hayo mawili unavyokwenda kwa kasi na kuwaeleza kuwa majengo hayo ni kwa ajili ya wafanyabiashara hivyo lazima wawe sehemu ya mradi.
Aidha amefurahishwa na ushirikiano uliotolewa na wafanyabiashara hao ikiwemo kupisha kwa hiyari yao eneo ambalo linafanyika ujenzi wa soko hilo na kuwahakikishia kuwa Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dkt. John Magufuli iko pamoja nao.
"Ninawapongeza sana wafanyabishara kwa moyo mliouonyesha, mmekaa pembeni hamna shida najua mnasubiri kwa hamasa kubwa kukamilika kwa jengo hili ili muweze kufanya biashara zenu. Kikubwa napita kwa ajili ya kujiridhisha na kile kinachoendelea ili tusije kujenga miundombinu ambayo sio rafiki kwenu.” Amesisitiza.
DC amewaeleza wafanyabiashara hao kuwa Mhe. Rais Dkt. John Magufuli ametoa zaidi ya shilingi bilioni 18 kwaaajili ya ujenzi wa masoko hayo mawili ya Tandale na Magomeni ili kuboresha mazingira ya wao kufanyia biashara.
Akizungumzia soko la Tandale ambalo linauwezo wa kuchukua wafanyabishara zaidi ya 1,000 Mhe. Chongolo amesema kuwa kulingana na idadi hiyo kubwa ambayo wengi wana matamanio ya kufanya shughuli zao kwenye ghorofa ya chini, wana angalia namna ya kutengeneza mazingira ili wote waweze kupata eneo bila kuwepo na malalamiko.
Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.