Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mheshimiwa Songoro Mnyonge, Agosti 23,2024 ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita, Kwa kuuendeleza na kuukamilisha wa mradi wa ujenzi wa daraja la linalounganisha kati ya Busisi na Kigongo, Mkoani Mwanza.
Mheshimiwa Songoro alitoa pongezi hizo wakati wa ziara ya Waheshimiwa Madiwani na baadhi ya Watendaji wa Manispaa ya Kinondoni yenye lengo la kubadilishana uzoefu katika Usimamizi wa Miradi, usafi wa miji, uwezeshaji makundi maalum na ukusanyaji mapato.
Ziara hiyo inafanyika katika Jiji la Mwanza ambapo pia ameelezea haja ya kuanzisha ushirikiano baina ya Halmashauri hizo mbili.
Akiwa katika mradi huo wa daraja, Mheshimiwa Songoro alisema kuwa, "Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kutekeleza mradi huo vizuri. Huu ni mradi wa kitaifa, Sisi tumekuja kujionea ili tuweze kuusemea Kwa wananchi namna Serikali inavyoutekeleza."
Daraja hilo linatarajiwa kukamilika Desemba 30, 2024 ili lianze kutumika ambapo pamoja na kuunganisha mikoa ya Kanda ya Ziwa na Magharibi, pia litaiunganisha Tanzania na nchi za ukanda wa Maziwa Makuu.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.