Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Bi. Hanifa Suleiman Hamza, amewataka wakazi wa Kinondoni waliopo kwenye maeneo hatarishi kuchukua tahadhari dhidi ya mvua zinazoendelea kunyesha.
Rai hiyo aliitoa leo April 26, 2024 wakati alipotembelea maeneo yote yaliyokumbwa na maji sambamba na kutoa pole kwa wahanga wa maeneo hayo.
Alisema, "Poleni sana kwa majanga haya. Lakini nawaomba sana muendelee kuchukua tahadhari pindi mnapoona mvua imezidi ili kuepuka kutokea kwa madhara makubwa."
Kadhalika, Mkurugenzi Hanifa aliwataka Wenyeviti wa Mitaa kuendelea kuwapa elimu na kuwahamasisha Wananchi kuchukua tahadhari kwenye maeneo yao ikiwemo wazazi kuwa makini kwa watoto wao katika kipindi hiki.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.