Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kupitia Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi imeanza zoezi la utoaji wa chanjo ya kichaa cha Mbwa na Paka katika Kata zote 20.
Akiongea katika zoezi hilo Kaimu Mkuu wa Divisheni hiyo Bi. Betila Lyimo amesema kwa siku ya leo jumla ya Mbwa 85 na Paka 07 wamepatiwa chanjo na huduma ya kuogeshwa, hivyo Wananchi wanatakiwa kuendelea kuwaleta Mbwa wao kupatiwa chanjo kwani zoezi hili litadumu wiki nzima.
"Kichaa cha Mbwa hakina tiba, hivyo tuzingatie kinga zinazotolewa kupitia chanjo zinazoelekezwa na Wataalamu wetu " amesema Mhe Lukindo.
Aidha, Diwani wa Kata ya Mbezi Juu Mhe. Anna Lukindo amewaomba Wafugaji na Wamiliki wa Mbwa na Paka kuhakikisha wanapatiwa chanjo hiyo itakayotolewa bure kwa muda wa siku saba.
Mheshimiwa Anna amesema hayo Septemba 28, 2024 katika Maadhimisho ya Siku ya Kichaa cha Mbwa Duniani, ambapo Manispaa ya Kinondoni imeadhimisha Kata ya Mbezi Juu Kiwilaya.
"Tukiendelea kuwapatia chanjo Wanyama hawa tutakuwa tunatimiza matakwa ya kauli mbiu isemayo, Ondoa vikwazo na vizingiti vinavyorudisha nyuma mapambano dhidi ya ugonjwa wa kichaa cha Mbwa " Mhe. Diwani.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.