VYAMA vya Siasa Wilaya ya Kinondoni Januari 29, 2024 vimeipongeza Manispaa ya Kinondoni kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2023/2024.
Pongezi hizo zimewasilishwa wakati wa Kikao cha Baraza la Ushauri la Wilaya lililoketi kwa ajili ya kujadili na kupitisha bajeti ya Manispaa ya Kinondoni kwa mwaka 2024/2025.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia Makini, Mheshimiwa Costa Kibonde, alisema, "tunapongeza kwa dhati utekelezaji wa miradi ya maendeleo ndani ya Manispaa yetu lakini pia kwa namna ambavyo Serikali ya Awamu ya Sita inavyotekeleza miradi ya maendeleo."
Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Mheshimiwa Shaweji Mkumbule, alisema kuwa "CCM tunaunga mkono mapendekezo ya bajeti hii na tunaomba utekelezaji wake uwe mzuri kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo yao."
Manispaa ya Kinondoni imewasilisha katika Baraza hilo mapendekezo ya bajeti ya jumla ya Shilingi 149,456,590,400.00 ambapo Manispaa inatarajia kukusanya mapato ya ndani ya Shilingi 74,200,154,000.00 huku ikitarajia kupokea Ruzuku kutoka Serikali Kuu Shilingi 75,256,436,400.00.
Bajeti ya mwaka 2024/2025 inaongezeko la asilimia Nane kutoka bajeti ya Mwaka 2023/2024 kwa Shilingi 11,268,407, 000.00.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.