Zaidi ya Shilingi za Kitanzania bilioni 6.7 zimetumika kutoa mikopo kwa vikundi 771 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika mwaka wa fedha 2021/2022 ndani ya Manispaa ya Kinondoni.
Kati ya vikundi hivyo, vikundi 564 vya wanawake vilipokea jumla ya Shilingi za Kitanzania 3,442,173,000.00 wakati vikundi 173 vya vijana vilipokea jumla ya Shilingi za Kitanzania 2,809,337,333.00 na vikundi 34 vya watu wenye ulemavu vilipokea mikopo yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania 513,600,000.00.
Taarifa ya mikopo hiyo imetolewa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mheshimiwa Songoro Mnyonge, wakati wa mahojiano maalum ofisini kwake. Mikopo hiyo inayotokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani ambapo kwa mwaka huo wa fedha Manispaa iliweza kukusanya zaidi ya Shilingi za Kitanzania bilioni 57 za mapato ya ndani.
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini:
Manispaa ya Kinondoni
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.