Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imetenga kiasi cha shilingi bilioni 5.2 kwa ajili ya mikopo ya asilimia 10 kwa wajasiriamali kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Bw. Jabir Chilumba, aliyasema hayo wakati wa ufungaji wa maonyesho ya Majukwaa ya uwezeshaji wa wanawake kiuchumi Wilaya ya Kinondoni Novemba 24,2023 katika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam.
Bwana Jabir alisema, "Kwa mwaka huu wa fedha 2023/2024 Manispaa ya Kinondoni imetenga kiasi cha shilingi bilioni 5.2 ikiwa ni mikopo ya kuwawezesha vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu." asilimia 2 na hii ni moja ya kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwawezesha na kuwainua akina mama kiuchumi," amesema Bw. Chilumba.
Aliwataka Wajasiriamali hao kuendele na uzalishaji wa bidhaa zao kutokana na Serikali kuwaunga mkono na kwamba, "Manispaa ya Kinondoni itaendelea kuwashika mkono na kuwatafutia masoko ndani na nje ya nchi."
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.