Kamati elekezi ya usimamizi wa maafa kutoka Wilaya ya Kinondoni ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Saad Mtambule amefanya ziara katika ujenzi wa daraja la mto Mpiji lenye thamani ya Shilingi billioni 18.
Akiongea katika ziara, Mhe. Mtambule amesema ujenzi wa daraja linalounganisha eneo la Mbweni Mpiji na Mtaa wa Kiembeni litasaidia kwa kiasi kikubwa uendeshwaji wa shughuli za kimaendeleo ndani ya Wilaya yetu na taifa kwa ujumla.
Aidha, Mkuu wa Wilaya amewasisitiza Wananchi wa eneo hilo kuwa walinzi wa miundombinu ya daraja hilo pindi litakapokamilika kwani fedha zote za ujenzi huo ambazo zimetolewa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan hivyo ni wajibu kuvilinda kwa manufaa yao.
"Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametupatia bilioni 18 kwa ajili ya ujenzi wa daraja hili, hivyo ni wajibu wetu kuilinda miundombinu ya daraja hilo dhidi ya waharifu wote wenye nia ovu ya kuteketeza miundombinu ya Serikali na sisi hatutasita kuwachukulia hatua kali dhidi yao," amesema Mhe. Mtambule.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.