Sherehe hizo zinazoambatana na kauli mbiu isemayo "familia na jamii tuwajibike kuwatunza wazee" zinatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi Tar 3 Oktoba katika viwanja vya Mnazi mmoja yakiwa ni makubaliano yaliyofikiwa leo katika kikao cha robo ya kwanza ya mwaka 2020-2021 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa .
Akitoa hoja hiyo katika katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Baraza hilo Bw Wallace K. Mwakikalo amesema huo utakuwa wakati mzuri kwao kutoa matamko ya pamoja na kuweka mipaka ya kimajukumu kati ya mabaraza ya wazee na vikundi mbalimbali vya kusaidia wazee.
Ameongeza kuwa katika maadhimisho hayo pia itakuwa ni nafasi pekee ya kupanga mikakati yao ya kupambana na changamoto zinazowakabili pamoja kama Mkoa na kubadilishana uzoefu.
" Kumekuwa na changamoto ya muingiliano wa majukumu Kati ya baraza la wazee na hivi vikundi vya kijamii vinavyofanya kazi na jamii ya wazee, huu utakuwa wakati mzuri kwetu kutoa tamko la mipaka ya kimajukumu tukiwa na viongozi wetu wa mkoa wa Dar es salaam"
Kwa upande wake Katibu wa Baraza hilo Bi Neema Mwalubilo amesema Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika tarehe 3 mwezi ujao katika viwanja vya mnazi mmoja ambapo wazee wa kinondoni watajumuika na wazee wengine katika kuhadhimisha siku yao muhimu.
Naye Afisa ustawi wa Manispaa ya Kinondoni Bi.Judith Kimaro amelitaka Baraza hilo kuwa balozi kwa wazee kujiunga na mfuko wa (ICHF), ili wawe na uhakika wa matibabu pale wanapoumwa na wazee hao kuwa mabalozi wazuri kwa wenzao wasio na uwezo wa kupata matibabu kwa kuwasaidia waweze kupatiwa kadi za msamaha wa matibabu.
Imeandaliwa na
kitengo cha habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.