Baraza la Madiwani robo ya tatu kipindi cha Januari hadi Machi 2022 limefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Manispaa.
Akifungua mkutano huo uliohudhuriwa pia na Wakuu wa Idara na Vitengo, Mwenyekiti wa Baraza ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Songoro Mnyonge amesema ni mkutano wa kawaida kwa lengo la kuthibitisha taarifa za kawaida za utekelezaji wa Kamati za Kudumu za Halmashauri.
Amesema taarifa hizi ni za utekelezaji kwa kipindi cha robo ya tatu na zitawasilishwa na Wenyeviti wa Kamati hizo za Kudumu kwa lengo la kuzijadili ili changamoto ziweze kutatuliwa kwa wakati na ufanisi.
Taarifa zilizowasilishwa ni utekelezaji wa Kamati ya Maadili ya Madiwani, Kamati ya Huduma za Uchumi Afya na Elimu, Kamati ya Mipangomiji na Mazingira, Kamati ya Kudhibiti UKIMWI pamoja na Kamati ya Fedha na Uongozi.
Pamoja na kuwasilishwa kwa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, Meya Songoro ameitaka Halmashauri hiyo kuhakikisha inasimamia vema miradi ya maendeleo katika sekta ya elimu, afya, barabara, maji na miundombinu mingine ili kuleta tija kwa Halmashauri na wananchi kwa ujumla.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndg Shedrack Maximilian alipofafanua ameahidi kutekeleza maelekezo yaliyotolewa ili kuleta tija kwa Halmashauri.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.