Baraza hilo chini ya Mwenyekiti wake Mhe.Songoro Mnyonge limeipitisha taarifa hiyo ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo robo ya kwanza Julai hadi Septemba 2020/2021 katika kikao cha baraza kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa.
Akipitisha taarifa hiyo Mhe.Songoro amesema taarifa hii ya utekelezaji ni ile ya bajeti inayomalizika miezi michache ijayo hivyo imetekelezwa kwa kiwango cha kuridhisha na kuwataka Madiwani kuorodhesha mahitaji yao katika bajeti ijayo ya 2021/2122.
"Mimi niwashauri Wahe.Madiwani bajeti tunayotekeleza sasa tumeikuta, imebakiza miezi michache, lakini mchakato wa kuandaa bajeti ijayo tayari umeshaanza katika ngazi ya Halmashauri, hivyo niwaombe Wahe.madiwani twende tukapitie mipango yetu ili tuiingize kwenye mpango wa bajeti" Amesema Mstahiki.
Akiwasilisha taarifa hiyo ya utekelezaji katika kikao cha Baraza hilo Katibu wa kikao hiko ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Ndg Aron Kagurumjuli amesema kwa mwaka wa fedha 2020/2021 Manispaa ilipanga kutumia jumla ya shilingi takribani Bilioni 30.5 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Amesema fedha hizo zimetokana na vyanzo mbalimbali na kuvitaja kuwa ni mapato ya ndani ya Halmashauri, ruzuku kutoka Serikali kuu pamoja na nguvu ya jamii.
Katika kikao hicho cha baraza Wahe.Madiwani ambao ni wenyeviti wa kamati za kudumu pia walipata fursa ya kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa shughuli za kamati zao.
Taarifa zilizowasilishwa katika baraza hilo ni za kamati za kudumu robo ya kwanza Julai hadi Septemba 2020/2021 ambazo ni taarifa za huduma za Uchumi afya na Elimu, taarifa za kamati ya mipangomiji na mazingira, taarifa za kamati ya kidhibiti UKIMWI, taarifa za Kamati ya maadili na taarifa za Kamati ya fedha na Uongozi.
Imeandaliwa na:
Kitengo Cha Habari na Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.